Luke 3

Yahya Mbatizaji Aanza Kuhubiri

(Mathayo 3:1-12; Marko 1:1-8; Yohana 1:19-28)

1 aKatika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato akiwa mtawala wa Uyahudi, Herode akiwa mfalme wa Galilaya, Filipo ndugu yake akiwa mfalme wa Iturea na nchi ya Trakoniti, na Lisania akiwa mfalme wa Abilene, 2 bnao Anasi na Kayafa wakiwa makuhani wakuu, neno la Mungu likamjia Yahya, mwana wa Zekaria huko jangwani. 3 cAkaenda katika nchi yote kandokando ya Mto Yordani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi. 4 dKama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Sauti ya mtu aliaye nyikani,
‘Itengenezeni njia ya Bwana,
yanyoosheni mapito yake.

5 Kila bonde litajazwa,
kila mlima na kilima vitashushwa.
Njia zilizopinda zitanyooshwa,
na zilizoparuza zitasawazishwa.

6 eNao watu wote watauona
wokovu wa Mungu.’ ”

7 fYahya akauambia ule umati wa watu uliokuwa unakuja ili kubatizwa naye, “Ninyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu inayokuja? 8 gBasi zaeni matunda yastahiliyo toba. Wala msianze kusema mioyoni mwenu kuwa, ‘Sisi tunaye Ibrahimu, baba yetu.’ Kwa maana nawaambia kuwa Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto kutoka mawe haya. 9 hHata sasa shoka limeshawekwa tayari kwenye shina la kila mti. Basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.”

10 iUle umati wa watu ukamuuliza, “Inatupasa tufanyeje basi?”

11 jYahya akawaambia, “Aliye na kanzu mbili amgawie asiye nayo, naye aliye na chakula na afanye vivyo hivyo.”

12 kWatoza ushuru nao wakaja ili wabatizwe, wakamuuliza, “Bwana na sisi inatupasa tufanyeje?”

13 lAkawaambia, “Msichukue zaidi ya kiwango mlichopangiwa.”

14 mAskari nao wakamuuliza, “Je, nasi inatupasa tufanye nini?”

Akawaambia, “Msimdhulumu mtu wala msimshtaki mtu kwa uongo, bali mridhike na mishahara yenu.”

15 nWatu walikuwa na matazamio makubwa. Wakawa wanajiuliza mioyoni mwao iwapo Yahya angeweza kuwa ndiye Al-Masihi.
Al-Masihi maana yake ni Masiya , yaani Aliyetiwa mafuta.
16 pYahya akawajibu akawaambia, “Mimi nawabatiza kwa maji.
Tafsiri nyingine zinasema ndani ya maji.
Lakini atakuja aliye na nguvu kuniliko mimi, ambaye sistahili hata kufungua kamba za viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
17 rPepeto lake liko mkononi, tayari kusafisha sakafu yake ya kupuria na kuikusanya ngano ghalani, lakini makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.” 18Basi, kwa maonyo mengine mengi Yahya aliwasihi na kuwahubiria watu Habari Njema.

19 sLakini Yahya alipomkemea Mfalme Herode kuhusu uhusiano wake na Herodia, mke wa ndugu yake, na maovu mengine aliyokuwa amefanya, 20 tHerode aliongezea jambo hili kwa hayo mengine yote: alimfunga Yahya gerezani.

Kubatizwa Kwa Bwana Isa

(Mathayo 3:13-17; Marko 1:9-11)

21 uBaada ya watu wote kubatizwa, Isa naye akabatizwa. Naye alipokuwa akiomba, mbingu zilifunguka. 22 vRoho Mtakatifu akashuka juu yake kwa umbo kama la hua, nayo sauti kutoka mbinguni ikasema: “Wewe ni Mwanangu mpendwa; nami nimependezwa nawe sana.”

Ukoo Wa Bwana Isa

(Mathayo 1:1-17)

23 wIsa alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoanza huduma yake. Alikuwa akidhaniwa kuwa mwana wa Yusufu,

Yusufu alikuwa mwana wa Eli,

24 Eli alikuwa mwana wa Mathati,
Mathati alikuwa mwana wa Lawi,
Lawi alikuwa mwana wa Melki,
Melki alikuwa mwana wa Yanai,
Yanai alikuwa mwana wa Yusufu,

25 Yusufu alikuwa mwana wa Matathia,
Matathia alikuwa mwana wa Amosi,
Amosi alikuwa mwana wa Nahumu,
Nahumu alikuwa mwana wa Esli,
Esli alikuwa mwana wa Nagai,

26 Nagai alikuwa mwana wa Maathi,
Maathi alikuwa mwana wa Matathia,
Matathia alikuwa mwana wa Semeini,
Semeini alikuwa mwana wa Yoseki,
Yoseki alikuwa mwana wa Yoda,

27 xYoda alikuwa mwana wa Yoanani,
Yoanani alikuwa mwana wa Resa,
Resa alikuwa mwana wa Zerubabeli,
Zerubabeli alikuwa mwana wa Shealtieli,
Shealtieli alikuwa mwana wa Neri,

28 Neri alikuwa mwana wa Melki,
Melki alikuwa mwana wa Adi,
Adi alikuwa mwana wa Kosamu,
Kosamu alikuwa mwana wa Elmadamu,
Elmadamu alikuwa mwana wa Eri,

29 Eri alikuwa mwana wa Yoshua,
Yoshua alikuwa mwana wa Eliezeri,
Eliezeri alikuwa mwana wa Yorimu,
Yorimu alikuwa mwana wa Mathati,
Mathati alikuwa mwana wa Lawi,

30 Lawi alikuwa mwana wa Simeoni,
Simeoni alikuwa mwana wa Yuda,
Yuda alikuwa mwana wa Yusufu,
Yusufu alikuwa mwana wa Yonamu,
Yonamu alikuwa mwana wa Eliakimu,
Eliakimu alikuwa mwana wa Melea,

31 yMelea alikuwa mwana wa Mena,
Mena alikuwa mwana wa Matatha,
Matatha alikuwa mwana wa Nathani,
Nathani alikuwa mwana wa Daudi,

32 zDaudi alikuwa mwana wa Yese,
Yese alikuwa mwana wa Obedi,
Obedi alikuwa mwana wa Boazi,
Boazi alikuwa mwana wa Salmoni,
Salmoni alikuwa mwana wa Nashoni,

33 aaNashoni alikuwa mwana wa Aminadabu,
Aminadabu alikuwa mwana wa Aramu,
Aramu alikuwa mwana wa Hesroni,
Hesroni alikuwa mwana wa Peresi,
Peresi alikuwa mwana wa Yuda,

34 abYuda alikuwa mwana wa Yakobo,
Yakobo alikuwa mwana wa Isaka,
Isaka alikuwa mwana wa Ibrahimu,
Ibrahimu alikuwa mwana wa Tera,
Tera alikuwa mwana wa Nahori,

35 Nahori alikuwa mwana wa Serugi,
Serugi alikuwa mwana wa Reu,
Reu alikuwa mwana wa Pelegi,
Pelegi alikuwa mwana wa Eberi,
Eberi alikuwa mwana wa Sala,

36 acSala alikuwa mwana wa Kenani,
Kenani alikuwa mwana wa Arfaksadi,
Arfaksadi alikuwa mwana wa Shemu,
Shemu alikuwa mwana wa Nuhu,
Nuhu alikuwa mwana wa Lameki,

37 adLameki alikuwa mwana wa Methusela,
Methusela alikuwa mwana wa Idrisi,
Idrisi alikuwa mwana wa Yaredi,
Yaredi alikuwa mwana wa Mahalaleli,
Mahalaleli alikuwa mwana wa Kenani,

38 aeKenani alikuwa mwana wa Enoshi,
Enoshi alikuwa mwana wa Sethi,
Sethi alikuwa mwana wa Adamu,
Adamu alikuwa mwana wa Mungu.
Copyright information for SwhKC